Chuo kikuu cha Lagos nchini Nigeria kimepiga marufuku wanafunzi kuvaa nguo zinazobana mwili wakati wakiwa chuoni hapo.
Taarifa iliyotolewa kwa wanafunzi chuoni hapo imesema kuwa wanafuzni hao wanapaswa kuonekana nadhifu wawapo katika maeneo ya chuo, na kwamba uvaaji wa nguo za kubana ama zinazoonesha miili yao, sio jambo la kufaa.
Chuo kimepiga marufuku nguo zote ambazo zinaonesha maeneo nyeti ya sehemu za mwili kama vile kifua, tumbo, sehemu ya matiti, makalio.
Raia wengi wa Nigeria wamekuwa wakipendelea kuvaa nguo zenye staha, lakini katika kizazi cha vijana wa sasa mara nyingi wamekuwa wakidharau maadili ya mavazi ya asili.