Nahodha wa Bayern Munich, Philipp Lahm ametangaza kustastaafu soka mwishoni mwa msimu huu baada ya kucheza kwa miaka kumi na tano.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 33 ametangaza uamuzi huo baada ya Bayern kushinda mechi ya hatua ya 16 bora katika michuano ya Kombe la Ujerumani dhidi ya Wolfsburg.

Lahm ambaye pia alikuwa nahodha wa timu ya taifa ya Ujerumani walipotwaa Kombe la Dunia mwaka 2014 nchini Brazili baada ya kuwafunga Argentina.

Hii ina maana kwamba ataondoka klabu hiyo mwaka mmoja kabla ya mkataba wake kumalizika.

Lahm alianza kucheza mechi yake ya kwanza katika kikosi cha wachezaji wakubwa wa Bayern mwaka 2002 na ameshinda mataji saba ya Bundesliga akiwa na klabu hiyo, pamoja na Kombe la Ligi ya Klab

Baada ya kuingoza Ujerumani kutwaa kombe la dunia nchini Brazil beki huyo alitangaza kustaafu soka la kimataifa na sasa ametangaza kustaafu soka kwa ujumla.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *