Wabunge nchini Somalia leo wanapiga kura kumchagua rais wa nchi hiyo kwenye uchaguzi wa nchi hiyo.
Uchaguzi huo umebadilika kutokana na kutokuwa na daftari la wapiga kura ambapo wabunge mia tatu na ishirini na tisa ndio watakaomchagua Rais mpya.
Wanawake wengi zaidi watashiriki kupiga kura wakati huu, hivyo kufanya asilimia ishirini na sita ya kura zote za bunge.
Ingawa wanawake wawili waliotangaza nia ya kuwania Urais akiwemo Fatuma Dayyib aliyetangazwa sana, walijitoa.
Licha ya maswali mengi kuhusu uchaguzi huu, wananchi wa Somalia wanatumai kuwa kufanikiwa kwa uchaguzi huu utawaongoza kwenye uchaguzi mkuu mwaka 2020.
Mahali pa kufanyia uchaguzi pamehamishwa, kutoka Chuo cha Polisi hadi Uwanja wa ndege wa Mogadishu wenye ulinzi mkali kutokana na kuongezeka kwa vitisho vya usalama na rushwa .
Hivi leo ndege hazitaruhusiwa kutua au kupaa kutokea uwanja huu, kwa kuwa ni siku ya kupiga kura.