Mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulika na kuzuia mauaji ya watu wengi, Adama Dieng amesema zaidi ya watu elfu 52 wamekimbilia nchini Uganda katika kipindi cha mwezi mmoja uliopita.
Adama Dieng mesema hali ilivyo katika mji wa Kajo -keji ulioko kusini mwa mji mkuu wa nchi hiyo Juba, ambako kikosi cha Walinzi wa Usalama wa Umoja wa Mataifa walifika huko siku ya Jumapili.
Baada ya kupata uhuru wake mwaka 2011 Sudan ya kusini iliingia katika vita vya wenyewe kwa wenyewe mwaka 2013 na kusababisha watu takriban milioni tatu kuyakimbia makazi.
Zaidi ya watu milioni sita, nusu ya idadi ya watu wa nchi hiyo inasemekana wanahitaji msaada wa haraka.