Mshambuliaji wa zamani wa klabu ya Liverpool ya Uingereza na timu ya taifa ya Ufaransa, Djibril Cisse amestaafu soka akuwa na miaka 35.
Cisse ambaye aliichezea Liverpool kati ya mwaka 2004 na 2007 ameamua kustaafu kutokana na kushindwa kurejea uwanjani licha ya kufanyiwa operesheni ya paja.
Cisse ambaye amecheza soka kwa miaka 17 ameamua kutundika daruga baada ya klabu aliyoanza kuchezea soka la kulipwa ya Auxere kushindwa kumpa mkataba.
Cisse sasa ameamua kugeukia kazi ya kuchezesha muziki, kutengeneza muziki na kuwa mchambuzi wa soka.
‘Nimekuwa ninapenda kuwa mcheza soka, mpaka kufikia sasa, mpira ndo umekuwa maisha yangu. Ningependa kuendelea na soka lakini napaswa kukiri kuwa, soka ndo limeishia hapa’.
Cisse aliichezea timu ya taifa ya Ufaransa mara 41 huku akivichezea pia vilabu vya Sunderland, Panathinaikos, Lazio, QPR, Kuban Krasnodar na Bastia.