Staa wa Pop wa Marekani, Lady Madonna amefanikiwa kuasili watoto wengine wawili nchini Malawi baada ya mahakama ya Lilongwe kumpa ruhusa ya kuchukua watoto hao mapacha.

Shirika la utangazaji la AFP, limeripoti kuwa staa huyo alikuwa mahakamani jijini Lilongwe siku ya leo kwaajili ya kusikiliza uamuzi wa mahakama juu ya ombi hilo.

Mnamo tarehe 25 Jnuari, Madona alikanusha kuwasilisha maombi ya kuasili watoto wengine baada ya msemaji wa serikali ya Malawi kudai kuwa muimbaji huyo amewasilisha maombi ya kuasili watoto wengine.

Madonna aliasili mtoto wa kwanza nchini Malawi mwaka 2006 kisha kuasili mwingine mwaka 2009.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *