Kampuni 30 zaidi za teknolojia nchini Marekani zimetia saini muhtasari wa kupinga sheria ya rais Donald Trump kuhusu uhamiaji na kuyafanya makampuni hayo kwa jumla kufikia 127.
Makampuni yaliyoongezeka kwenye orodha hiyo ni pamoja na Tesla, Adobe, HP na Evernote.
Wameunagana na makampuni mengine 97 ambayo yalifungua jalada la kisheria kueleza kuwa sheria mpya iliyotiwa saini na rais Rtump ‘inasababisha athari kubwa’ kwenye biashara zao na ni sheria iliyo kinyume cha katiba.
Muhtasari wa mshauri wa mahakama asiyefungamana na upande wowote unaruhusu kampuni au watu wasiohusika moja kwa moja na kesi lakini wanaoona wanaathiriwa na lalalmiko lililopo mahakamani, kutoa maoni yao.
Shauri hilo lililofunguliwa Jumapili iliyopita pia linazihusu kampuni za Apple, Facebook na Microsoft kama watia sahihi kwa niaba ya makampuni mengine.