Leo ni maadhimisho ya siku ya kimataifa ya elimu kuhusu ukeketaji ‘international female genital mutilation (FGM) awareness day’.

Kampeni hii inadhaminiwa na Umoja wa Mataifa (UN) ambayo program zake kuhusiana na ukeketaji zinalenga kuyaangazia mataifa 17 ya barani Afrika.

Inakadiriwa kuwa wasichana na wanawake milioni 200 walio hai ulimwenguni walifanyiwa kitendo cha ukeketaji.

Takwimu za Umoja wa Mataifa zinaonyesha kuwa nchi ambazo tatizo hilo ni kubwa zaidi ni miongoni mwa wanawake wenye umri wa kati ya miaka 15 na 49 ni Somalia kwa 98%, Guinea (97%) na Djibouti (93%).

Umoja wa Mataifa unatoa elimu ya namna ya watu kufanya ili kuondoa tatizo hilo kupitia matangazo ya ‘LIVE’ kwenye mtandao wa Facebook.

Hizi hapa ni takwimu za Umoja wa Mataifa na ufafanuzi wa kitaalamu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *