Wagombea wengi wa nafasi ya urais kwenye nchi ya Somalia wameshindwa kujitokeza kwenye mdahalo wa nafasi hiyo uliopangwa kurushwa kwenye luninga.

Wagombea watatu tu kati ya wagombea 11 ndio walioweza kujitokeza kunadi sera na mipango yao kwenye mdahalo huo huku wagombea wengine wakigomea mdahalo huo ambao ni wa kwanza katika historia ya nchi hiyo kurushwa kwenye luninga.

Wagombea urais wa nchi hiyo hadi kufikia leo hii wako 23 na mdahalo huo umewagawa katika makundi mawili ambapo kundi la pili ambamo yumo rais aliyepo madarakani Hassan Sheikh Mohamud, wagombea wake watashindana leo.

Uchaguzi mkuu nchini humo unatarajia kufanyika siku ya Jumatano huku mfumo wao wa uchaguzi ukiwataka viongozi 135 wa makabila ya nchini humo huwachagua watu 14,025 kuwachagua wabunge.

Wabunge hao na baraza la juu humchagua rais wa nchi hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *