Nahodha wa timu ya taifa ya Kriketi ya Uingereza, Alastair Cook amejiuzuru nafasi hiyo baada ya kuweka rekodi ya kucheza mechi 59 akiwa nahodha wa timu hiyo.
Mchezaji huyo wa timu ya Essex mwenye umri wa miaka 32 alikabidhiwa jukumu la unahodha mwaka 2012 na alikiongoza kikosi cha Uingereza kushinda mashindano ya Ashes mwaka 2013 na 2015.
Cook aliwahi kuweka wazi nia ya kujiuzuru wadhifa huo mwaka jana baada ya kichapo cha 4-0 kwenye Test series dhidi ya India aliposema ‘anajiuliza maswali juu ya wadhifa huo’.
‘Kujiuzuru umekuwa uamuzi mgumu sana kwangu lakini nafahamu ni uamuzi sahihi kwangu na kwa timu nzima’. Amenukuliwa Cook.
Cook ameweka rekodi ya kuwa nahodha wa Uingereza aliyefunga mikimbio mingi zaidi kwenye michezo ya Test akiwa na alama 11,057, na ushiriki wake wa mara 140 kwenye Test 140 na mara 30 za centuries pia ni rekodi kwa Uingereza.