Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Chege Chigunda amesema yuko mbioni kukata kiu ya mashabiki wao kwa kuandaa nyimbo mpya akiwa na Temba baada ya kukaa kimya bila ya kutoa ngoma wakiwa wawili.
Chege ameweka hilo wazi kutokana na kukumbana na maswali mengi ya watu mbalimbali wakitaka kujua ni lini wasanii hao watafanya tena kazi ya pamoja kutokana na temba kuwa kimya kwa muda mrefu.
Mkali huyo amesema kuwa kwa sasa na yeye ameamua kutoa albam kwa kuwa anaamini albam zina soko, na kwa kutambua wabongo wame-miss albam kwa muda mrefu, sasa ameamua kukata kiu ya mashabiki.
Ameitaja albam yake kuwa itakwenda kwa jina la ‘Sweet Sweet’ na itakuwa na nyimbo 15, na kwamba kila kitu kimekamilika na katikati ya mwezi huu itakua imeingia sokoni.