Klabu ya Yanga inatarajiwa kuondoka Ijumaa ijayo kwenda Comoro kwa ajili ya mchezo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya wenyeji, Ngaya Club.

Yanga inashiriki Ligi ya Mabingwa Afrika kwa mara ya pili mfululizo na inaanza na timu za Comoro baada ya mwaka jana kuanza na Cercle de Joachim kwenye mzunguko wa kwanza.

Kwa upande wa Azam FC ambao wao ushiriki kombe la Shirikisho Afrika itaanza kampeni yake dhidi ya timu ya mshindi kati ya Mbabane Swallows ya Swaziland na Opara United ya Botswana.

Yanga wataanzia ugenini Februari 10 hadi 12 kabla ya marudiano Februari 17 hadi 19, mwaka huu.

Azam wao wataanzia nyumbani Machi 10 hadi 12 na marudiano Machi 17 hadi 19 mwakani, 2017.

Yanga wakivuka hatua hiyo watakutana na mshindi kati ya Zanaco ya Zambia au APR ya Rwanda katika Raundi ya kwanza.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *