Mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali imeezua mapaa ya nyumba 61katika kata ya Nyegezi mkoani Mwanza na kuacha kaya 1394 za mitaa minane bila makazi kutokana na mvua hiyo.
Waathirika wa mvua hiyo wameiomba serikali kuwapa msaada wa haraka wa chakula na mahema kwa ajili ya kujisitiri na mvua zinazoendelea kunyesha mkoani humo.
Nyumba zilizoezuliwa mapaa yake kutokana na mvua hiyo ni za mitaa ya Ibanda relini,Pasua,Swila na Mnara wa Vodacom.
Afisa Mtendaji wa kata ya Nyegezi Charles Muso akatoa ushauri kwa wananchi kuhakikisha wanajenga nyumba imara.
Mkuu wa wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza Mary Tesha Onesmo ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya maafa wilayani humo mbali na kutembelea kaya zilizoathirika kwa mvua hiyo kwa ajili ya kuwapa pole,amesema serikali imetoa shilingi milioni tatu kwa familia hizo kwa ajili ya kujikimu,huku kila familia iliyopatwa na maafa hayo ikipatiwa kilo 15 za unga.