Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia chakula (FAO) limetoa onyo juu ya ongezeko la viwavi jeshi ambao huharibu mazao ya chakula.

FAO imeonya kuwa mlipuko wa wadudu hao kwenye nchi zaidi ya sita za Afrika unatoa taswira ya hatari kwa msimu wa chakula hivyo kutabiri huenda njaa iliyopo kwenye baadhi ya nchi hizo ikaongezeka.

Tayari nchi ya Zimbabwe imeshathibitisha kutokea kwa mlipuko wa wadudu hao ambao pia wanahisiwa kuwepo kwenye nchi za Malawi, Mozambique, Namibia, Afrika Kusini na Zambia.

Mlipuko huo ni hatari sana kwasababu tayari ukame uliozikumba baadhi ya nchi ikiwemo Zimbabwe na kuacha mamilioni ya watu wakiwa kwenye uhitaji mkubwa wa chakula.

FAO imetangaza kuitisha kikao cha haraka ndani ya siku 10 kwaajili ya kufanya mpango wa kukabiliana na hatari ya wadudu hao pamoja na kujadili namna ya kuwasaidia raia wenye uhitaji mkubwa wa chakula.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *