Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Vanessa Mdee amejumuishwa kwemye orodha ya wanamuziki wanohusishwa na sakata la madawa ya kulevya.
Vanessa amejumuishwa kwenye orodha hiyo na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna Simon Sirro na kumjumuisha kwenye orodha iliyotajwa jana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.
Kamanda Sirro ameyasema hayo leo wakati akitoa taarifa kuhusu wasanii walioitikia wito wa RC Makonda aliyewataka wasanii na askari polisi 9 aliowataja kutuhumiwa kuhusika na biashara hiyo wafike katiika Kituo Kikuu cha Polisi Dar leo kwa ajili ya Mahojiano.
Vanessa Mdee anatakiwa kuripoti katika Kituo cha polisi siku ya Jumatatu ijayo kwa ajili ya mahojiano zaidi.
Sirro ameeleza kuwa ni watu watano tu ambao ni wasanii na raia wa kawaida ndiyo wameripoti leo kati ya wale waliotajwa jana na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam.