Rais wa Angola, Eduardo dos Santos amesema kuwa atastaafu urais wa nchi hiyo mwaka huu baada ya kutawala taifa hilo kwa kipindi cha miaka 38.

Eduardo dos Santos amelaumiwa kwa utawala wa kiimla baada ya kumteua mwanawe Isabel dos Santos kuwa mkuu wa kampuni ya mafuta ya serikaki Sonangol.

Isabel ambaye ni mwanamke tajiri zaidi barani Afrika akiwa na mali ya thamani ya dola bilioni 3.3 ni mkuu wa kampuni ya mafuta ya Serikali hadi sasa.

Waakilishi wa Bi Santos wanakana madai kuwa utajiri wake umetokana na wadhifa wa babake kama rais wa Angola.

Rais Eduardo amesema kuwa waziri wa ulinzi nchini Angola Joao Lourenco, mwenye umri wa miaka 62, atakuwa mgombea wa urais wa chama cha MPLA kwenye uchaguzi wa mwezi Agosti.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *