Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Ali Mohamed Shein amewataka viongozi na watendaji katika sekta ya umma kuacha kufanya kazi kwa mazoea.

Dk Shein amesema kuwa azma ya serikali ya kuwaongeza mshahara wafanyakazi wa kima cha chini ifikapo Aprili mwaka huu ipo pale pale.

Rais huyo ameyasema hayo kwenye wakati akifunga semina ya siku moja kwa viongozi na watendaji wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) kuhusu umuhimu wa takwimu na matumizi yake Mjini Unguja jana.

Pia amesisitiza haja kwa kila kiongozi kuhakikisha anasimamia vyema kazi zake pamoja na kuwasimamia anaowaongoza katika sehemu yake ya kazi pamoja na kufanya kazi kwa bidii na kuachana na kufanya kazi kwa mazoea.

Amesema ni jukumu la kila kiongozi kubadilika katika utendaji wake wa kazi na kuwataka wajitahidi kufanya hivyo licha ya kuwa itachukua muda, lakini aliwasisitiza kuwa si busara kuendelea kufanya kazi kwa mazoea.

Dk Shein amesema moja kati ya tamko la Ilani ya Chama cha ASP katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 1963 ilikuwa ni kuwapa nafasi Waafrika wa Zanzibar kuongoza nchi yao na baada ya Mapinduzi ya Januari 12, 1964 chini ya uongozi wa Mzee Abeid Amani Karume hilo lilifanikiwa kwa kuanzia Wizara ya Afya na kuendelea kwa wizara nyingine ambapo wananchi wa Zanzibar walipata.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *