Serikali imetoa onyo kali kwa gazeti la wiki la MwanaHALISI na kulitaka gazeti hilo, kuchapisha katika ukurasa wake wa mbele barua ya kuomba radhi baada ya kuchapisha taarifa iliyomhusisha Rais John Magufuli na ufisadi, uliofanywa katika Shirika la Elimu Kibaha.
Katika taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dk Hassan Abbasi, ilieleza kuwa barua hiyo ya kuomba radhi inatakiwa kuchapishwa katika toleo lijalo la gazeti hilo la Februari 6, mwaka huu.
Mkurugenzi huyo wa Maelezo amesema serikali imepokea barua ya MwanaHALISI ya kuomba radhi, iliyokiri upungufu katika habari hiyo na kwamba licha ya kukiri kwa makosa yao na kuchukua hatua hizo, imeamua kuchukua hatua hizo.