Rais Adama Barrow, amemchagua ‘mfungwa’ Amadou Sanneh kuwa waziri wa fedha wa nchi hiyo.
Sanneh ambaye alifungwa wakati wa utawala wa Yahya Jammeh ameachiwa huru na rais Barrow kisha kukabidhiwa mamlaka ya kuiongoza wizara ya fedha ya nchi hiyo.
Shirika la habari la Associated Press limedai kuwa saa 72 zilizopita (siku 3) Sanneh alikuwa bado gerezani lakini kwa sasa ndiye waziri wa fedha nchini humo.
Mbali na Sanneh pia mawaziri wengine walioapishwa na rais Barrow ni pamoja na mpinzani wa muda mrefu wa rais Jammeh Ousainou Darboe, ambaye pia aliwahi kuwa mfungwa wa kisiasa chini ya utawala wa Jammeh na kwa sasa ameukwaa uwaziri wa Mambo ya nje.
Ammadou Sanne alikuwa ndiye mhasibu mkuu wa taifa wa chama cha upinzani nchini humo cha United Democratic Party (UDP) ambacho kiliunganisha nguvu na vyama vingine na kumn’goa raias rais Jammeh kwenye uchaguzi wa mwezi Disemba mwaka jana.