Hisa zake zilipanda thamani kwa asilimia 2 baada ya biashara ya saa moja kufanikiwa zaidi kwenye mtandao huo.
Kwa upande mwingine mahakama nchini Marekani imeitaka kampuni hiyo ya facebook kuilipa dola milioni mia tano kampuni ya uchapishaji wa videogame ZeniMaxMedia kwa kutumia kodi ya kumpyuta yake ili kuzindua Virtual Reality Headset.
ZeniMax ilidai kwamba mfanyikazi wake mmoja wa zamani ambaye sasa ndio afisa mkuu wa maswala ya teknolojia katika facebook alianzisha teknolojia hiyo wakati bado alipokuwa akiifanyia kazi kampuni hiyo.