Staa wa filamu za Pirates of the Caribbean, Johnny Depp ameambiwa ajilaumu mwenye kwa matatizo ya kifedha yanayomkabili hivi sasa kwasababu alikuwa akiishi kifahari kwa bajeti ya $2m (TZS4.5bn) kwa mwezi.
Kwa mujibu wa mameneja wake wa fedha ambao ameamua kuwafungulia mashtaka ya kushindwa kusimamia vizuri pesa zake hivyo kudai fidia ya $25m (TZS25bn), staa huyo amekuwa na matumizi ya ‘kufuru’.
Wamedai kuwa alitumia zaidi ya $75m kununua nyumba 14.
Mameneja hao kupitia kampuni ya Management Group pia wamefungua kesi dhidi ya staa huyo.
Hati ya mashtaka dhidi ya staa huyo inaeleza kuwa: ‘Ameshindwa kuishi kulingana na kipato chake, licha ya…tahadhari za mara kwa mara kuhusiana na mwenendo wake wa kifedha’.
Pia hati hiyo inamtuhumu Depp kwa kutumia:
$18m (£14.3m) kununua boti ya kifahari yenye urefu wa futi 150
- $4m (£3.2m) kuwekeza kwenye biashara ya muziki iliyoshindwa kufanya vizuri
- $300,000 kwa mwezi kugharamia watumishi wa watu 40
- $200,000 kwa kutumia ndege binafsi
- $150,000 Kwa ulinzi binafsi
- $30,000 kununua na kuagiza mvinyo kutoka nje ya nchi
Pia staa huyo anadaiwa kuhitaji vyumba 12 kwaajili ya kuhifadhia kumbukumbu zake za kazi zake za Hollywood.
Mwezi uliopita, Depp alisema kuwa anaidai The Management Group zaidi ya $25m.
Pia Depp amewashtaki The Management Group kwa kushindwa kumpelekea taarifa zake za kodi kwa wakati hivyo kumsababishia hasara ya apoteze $5.7m kwa kulipia faini.
Depp ambaye sakata lake la kuvunjika kwa ndoa na mkewe Amber Hear limemalizika mwezi uliopita, anatarajiwa kuigiza tena kwenye filamu nyingine ya Pirates of the Caribbean: Salazar’s Revenge kama Captain Jack Sparrow.