Mwanajeshi wa Uingereza anayepigana vita nchini Syria, anadaiwa kujipiga risasi na kujiua kwa kuogopa kukamatwa mateka na wapiganaji wa kundi la IS.
Mwanajeshi huyo Ryan Lock aliyekuwa na umri wa miaka 20, anayetokea Chichester iliyopo jimbo la West Sussex, alifariki Disemba 21 wakati wa mapambano kwenye ngome ya IS kwenye mji wa Raqa.
Kwa mujibu wa taarifa ya wapiganaji wa kikurdi wa YPG ambao alijiunga nao mwezi Agosti, mwanajeshi huyo hakuuawa bali alijiua.
YPG wameliambia shirika la habari la BBC kuwa kidonda cha risasi iliyomuua Lock kimekutwa chini ya kidevu hivyo kuashiria kuwa alijiua.