Umoja wa Afrika (AU) umeunga mkono mpango wa kujiondoa kwa pamoja katika mahakama ya ICC ambayo mataifa mengi ya Afrika yanahisi inawalenga viongozi wa bara la Afrika pekee.

Uamuzi huo uliochukuliwa katika kikao cha faragha haujahalalisha hatua hiyo kilichofanyika katika makao makuu ya Umoja huo nchini Ethiopia.

Viongozi wa Afrika wamesema kuwa mahakama hiyo ilikosea kumlenga rais wa Sudan, Omar El Bashir kwa mauaji ya Darfur na Uhuru Kenyatta wa Kenya kwa kuchochea ghasia baada ya uchaguzi mkuu Nchini Kenya mwaka 2007.

Mpango huo umependekeza kwamba mataifa ya Afrika yanafaa kuimarisha mahakama zake na kupanua uwezo wa mahakama ya Afrika kuhusu haki na haki za binaadamu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *