Baada ya Idara ya Habari Maelezo kutoa masaa 24 kwa Gazeti la MwanaHALISI kumuomba radhi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli kutokana na kuchapisha habari yenye kichwa cha habari cha kumchafua rais hatimaye Gazeti hilo limeomba radhi.
Gazeti hilo linalotolewa na kampuni ya Hali Halisi lilichapisha kichwa cha habbari kilichosomeka “Ufisadi ndani ya ofisi ya JPM.
Idara ya Habari Maelezo katika taarifa yake ilisema kuwa kichwa cha habari hiko kinajenga dhana kuwa Rais Magufuli anahusika na kilichoitwa ufisadi wakati msingi wa taarifa husika ni tatizo la manunuzi katika Shirika la Elimu Kibaha!