Serikali ya India imekiri kuwa uamuzi wake ‘tata’ wa kuziondoa noti za rupia zenye thamani kubwa kwenye mzunguko mwishoni mwa mwaka jana kumekuwa na athari mbaya kwa uchumi wa nchi hiyo.

Jarida la taifa hilo la ‘Economic Survey’, limetoa taarifa inayoonyesha kuwa hatua hiyo imedororesha ukuaji wa uchumi wa nchi hiyo.

Hatua ya serikali ya India ya kuziondoa noti za rupia 500 (TZS16.53) na 1,000 iliyolenga kukabiliana na rushwa na kile kinachoitwa pesa chafu au umiliki usio halali wa pesa taslimu.

Hatua hiyo pia ilipelekea kuwepo kwa upungufu wa fedha ambao ulisababisha matatizo kwa watu binafsi na biashara.

Waziri wa fedha wa India, Arun Jaitley ambaye anatarajiwa kutoa hotuba ya Muungano kwenye mji wa Delhi amesema anatarajia uchumi utarudi kwenye hali ya kawaida kufikia mwezi Machi baada ya kusambazwa kwa pesa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *