Mwendesha mashtaka maarufu wa Afrika Kusini, ambaye alisimamia na kufanikiwa kumfungulia mashtaka ya mauaji mwanariadha mlemavu wa nchi hiyo, Oscar Pistorius na mkuu wa zamani wa polisi Jackie Selebi amejiuzuru.

Mwendesha mashtaka huyo, Gerrie Nel amekabidhisha barua ya kujiuzuru kwake wadhifa huo jana kwa kutoa taarifa ya saa 24.

Sababu ya Nel, ambaye kutokana na ukali wake na ujengaji wa hoja za nguvu mahakamani alipewa jina la ‘The Pitbull’ kujiuzuru nafasi hiyo bado haijawejwa wazi.

The Pitbull alipata umaarufu sana mwaka 2013 wakati alipofanikisha kufikishwa mahakamani kisha kushitakiwa kwa Oscar Pistorius kwa kosa la kumuua mpenzi wake Reeva Steenkamp.

Pia alisifika sana kwa kufanikisha kukamatwa na kufungwa kwa rais wa wakati huo wa Interpol, Selebi ambaye alikutwa na hatia ya kuchukua rushwa ya $156,000 (TZS349m) kutoka kwa mfanyabiashara wa dawa za kulevya Glenn Agliotti.

Ikiwa leo ndio siku yake ya mwisho kwenye ofisi ya Mamlaka ya Taifa ya Kuendesha Mashtaka inadaiwa kujiunga na taasisi ya wanaharakati wa haki za kiraia ambapo anatarajia kuanzisha kitengo cha uendeshaji mashtaka.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *