Baada ya kuikacha Taifa Stars, Charles Boniface Mkwasa ametangazwa rasmi kuwa Katibu Mkuu wa klabu Yanga.

Mkwasa mwenye taaluma ya ukocha daraja la kwanza la CAF, amewahi kuzifundisha klabu mbalimbali ikiwemo Yanga kwa vipindi tofauti na timu za taifa za wanaume na wanawake.

Mkwasa alikuwa kocha wa timu ya Taifa Stars kwa kipindi cha miezi 17 kabla ya TFF kusitisha mkataba wake mapema Januari 2017.

Makamu mwenyekiti wa klabu ya Yanga, Clement Sanga amemtambulisha Mkwasa leo mbele ya waandishi wa habari na kusema kocha huyo ambaye pia ni mchezaji wa zamani wa klabu hiyo, ameingia mkataba wa miaka miwili.

Mkwasa anachukua nafasi ya Baraka Deusdedit aliyekaimu nafasi hiyo kwa kipindi cha mwaka mmoja, kufuatia kuondoka kwa Jonas Tiboroha mapema mwanzoni mwa mwaka jana.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *