Kila mpanda ngazi hushuka na kila mchimba kaburi ‘HUINGIA MWENYEWE’.

Hakuna ukosefu wa hekima na busara kama kumkimbiza chizi anayeiba nguzo zako wakati unaoga kisha nawe ukaamua kutoka ‘kama ulivyozaliwa ili kumkimbiza’, ndo anachokifanya Diamond Platnumz.

Lakini hapa Bongo, hekima hii imeonekana kuwapitia mbali wengi.

Ingawa inawezekana kwa upande mmoja ikawa msanii anatafuta kiki lakini kila kiki ni lazima iwe na maana na impe mtu zaidi ya tija ya kupata ‘LIKES’ mtandaoni.

Diamond Platnumz ameonekana kuwa msanii ambaye sasa ‘hajielewi, kachanganyikiwa’.

Ni busara ndogo tu ambayo management yake inatakiwa kuifanyia kazi kuhakikisha Platnumz hapotezi wale anaosema anawapenda na kuwajali ‘mashabiki’.

Matusi ya nguoni anayotukana kwenye video aliyoifanyia mtandaoni ni ushahidi kuwa Platnumz ana ‘kibri’ na anapenda kuzungumzwa vizuri tu na inapotokea kinyume chake basi hana simile, hutoa MITUSI MIZITO.

Hii si mara ya kwanza kwa Diamond kufanya mambo ya aina hii ambayo hata hivyo yanatoa taswira mchanganyiko kwa wafuatiliaji wa burudani na kubwa zaidi kwa utamaduni wa kitanzania matendo haya yanamuweka kwenye kundi la watu ‘wasiojielewa’.

Aliwahi kumtukana matusi ya nguoni, Ommy Dimpoz.

Diamond ‘anatafuta kiki au anatafuta dhiki’?

‘Diamond anachimba kaburi la kwa kutumia umaarufu wake……….atauzika ustaa wake mwenyewe’

Hebu mtazame anachosema.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *