Sudan imepinga vikali katazo la rais wa Marekani, Donald Trump kuwapiga marufu raia wa nchi hiyo ambao wengi wao ni waislamu kuingia nchini Marekani.

Wizara ya mambo ya nchi za nje nchi hiyo imemuita balozi wa Marekani mjini Khartoum kupinga hatua hiyo ya kuwapiga marufuku raia wa nchi hiyo kuingia Marekani.

Sudan imesema kuwa hatua hiyo ni ishara mbaya baada ya hatua nzuri za kuboresha uhusiano wa mataifa hayo mawili ikiwemo kupunguza vikwazo vya kiuchumi na ushirikiano katika vita dhidi ya Ugaidi.

Amri hiyo ya Trump ilitikiza mpango mzima ya wakimbizi wa Marekani baada ya kutangazwa marufuku ya siku 90 ya usafiri wa raia kutoka Somalia, Sudan, Libya, Syria, Iran, Iraq na Yemen.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *