Meli mpya ya kisasa ‘AZAM SEALINK 2’ aina ya RORO yenye uwezo wa kubeba abiria wapatao 1650, mizigo uzito wa tani 717 sambamba na magari 150 imetia nanga kwa mara ya kwanza katika Bandari ya Tanga leo.

Meli hiyo inatarajiwa kufanya safari zake na kutoa huduma za kubeba abiria na mizigo ikiwemo magari kutoka Pemba kwenda Unguja hadi Tanga mara moja kwa wiki.

azam3

Meli hiyo inatarajiwa kupunguza adha ya uisafiri katika bandari hiyo sambamba na kurahisisha usafirishaji wa mizigo, magari pamoja na abiria kupitia Bandari ya Tanga.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *