Mrembo wa Ufaransa, Iris Mittebaere ameshinda taji la miss Universe kwenye fainali zilizofanyika katika mji wa Manila nchini Ufilipino jana usiku.
Mshindi huyo mwenye miaka 23 amefanukiwa kutwaa taji hilo lililoshirikisha washiriki 86 kutoka duniani kote na yeye kuibuka na ushindi huo.
Baada ya kutwaa taji hilo mrembo huo amewashukuru waandaaji wa shindano hilo la urembo pamoja na mashabiki zake waliojitokeza kumsapoti kwenye fainali hiyo iliyofanyika jana usiku na kuhudhuriwa na watu kibao.
Nafasi ya pili imekamatwa na Miss Haiti, Raquel Pelissier na ya tatu kwenda kwa Miss Colombia, Andrea Tovar.
Mittenaere amerithi taji hilo toka kwa mshindi wa mwaka jana, raia wa Ufilipino, Pia Wurtzbach.