Treni ya abiria yenye mabehewa tisa aina ya Deluxe, iliyokuwa ikitoka mkoani Kigoma kwenda Dar es Salaam imeanguka mkoani Pwani na kujeruhi watu kadhaa.

Katika mabehewa hayo, manne yameanguka, matatu yameacha njia na mawili yametenguka.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Boniventure Mushongi amesema kuwa mabehewa yaliyoanguka ni saba na kwamba wanaendelea kuwaokoa majeruhi.

Akizungumza kwa njia ya simu, Msemaji wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL), Midladjy Maez alisema ajali hiyo ilitokea saa 9:40 alasiri katika Kitongoji cha Kambini Ruvu Ngeta, Kata ya Kikongoa Wilaya ya Kibaha mkoani Pwani. Maez alisema mabehewa hayo yalianguka baada ya treni kuacha njia na kusababisha majeruhi kadhaa.

Alisema treni hiyo ilitakiwa ifike Dar es Salaam saa 11 jioni, lakini ilipofika hapo mabehewa hayo yalianguka na kusababisha kushindwa kuendelea na safari.

“Kutokana na ajili hiyo, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa na Mkurugenzi Mkuu wa TRL wanaelekea eneo la tukio ili kuweza kujua.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *