Kiungo wa Ufaransa, Dimitri Payet amekamilisha usajili wa kujiunga na klabu yake ya zamani, Marseille akitokea Westham kwa ada ya uhamisho Euro milioni 25.
Baada ya kukamilika kwa usajili huo West Ham United wamesema kuwa kiungo huyo nidhamu na upendo kwa timu hiyo baada ya kujiunga na klabu ya Marseille ya Ufaransa kwa Euro milioni 25.
Wagonga nyundo hao wa London wamesema kuwa hawakutaka kumuuza Payet huku mwenyekiti wa klabu hiyo David Sullivan akiongeza kuwa walitamani kuendelea kubaki nae.
Sullivan amesema kuwa sababu ya kumuuza ni ili kutokuondoa umoja wa wachezaji jambo ambalo ni muhimu zaidi.
Payet amejiunga na Marseille kwa mkataba wa miaka minne na nusu.