Wachimbaji madini 15 waliofukiwa na udongo mwekundu wa mgodini mkoani Geita wameokolewa wakiwa hai.
Miili yao haikuwa na nguvu, tumboni hakukuwa na kitu na njaa ya siku nne ilikuwa imewatafuna vilivyo kiasi cha kushindwa kusimama kwa miguu yao miwili baada ya kuokolewa
Baada ya zoezi la uokoaji, wachimbaji wote 15 waliokolewa jana hii katika mgodi huo wa dhahabu uliopo Nyarugusu mkoani Geita.
Baadhi yao, wakiongea kwa tabu walieleza kuwa, kukaa kwa siku nne kwenye kifusi hicho kuliwakatisha tamaa na kuzishuhudia siku zao za kuishi duniani zikikiyoyoma kila mshale wa saa ulivyokuwa ukitembea.