Jaji wa Marekani amesitisha matumizi ya sheria mpya iliyosainiwa na rais mpya wa Marekani, Donald Trump ambayo imeanza kutumikana kuathiri mamia ya raia wa kigeni wanaoishi nchini humo.
Chama cha kupigania haki za uraia nchini Marekani cha ‘The American Civil Liberties Union (ACLU)’ kilifungua kesi kwenye mahakama ya juu ili kupima kutekelezwa kwa sheria hiyo.
Kwa mujibu ACLU inakadiriwa kuwa kati ya watu 100 hadi 200 wanashikiliwa kwenye viwanja vya ndege au maeneo mengine ya kusafiria.
Maelfu ya watu wamekuwa wakiandamana nchini Marekani kupinga uamuzi wa rais Trump kusaini sheria inayowakandamiza wakimbizi.
Kwa kusainiwa sheria hiyo, shughuli zote za kuwasaidia wakimbizi zimesimamishwa nchin Marekani huku ikitoa zuio la siku 90 kwa raia yeyote kutoka nchi za Iran, Iraq, Libya, Somalia, Sudan, Syria na Yemen kutoingia Marekani.
Watu kutoka nchi hizo ambao wakati sheria hiyo inasainiwa walikuwa kwenye ndege kuelekea Marekani wamekuwa wakikamatwa kwenye viwanja vya ndege vya Marekani na kuzuiwa kutoendelea na safari hata kama wana vibali halali vya kuwaruhusu kuishi nchini humo.
Hukumu ya jaji, Ann Donnelly wa New York, imezuia uondolewaji wa watu wenye vibali halali vya kuishi Marekani vikiwemo viza zilizothibitishwa, watu wenye maombi ya ukimbizi yaliyothibitishwa na watu wengine ambao kisheria wana haki ya kuishi Marewkani’
Uamuzi huo wa kesi ya dharura pia umedai kuwa kuna hatari ya kutokea ‘maumivu yasiyoponyeka kwa wale watakaoathiriwa’.
Hata hivyo kesi hiyo itasikilizwa tena mwezi Februari.
Sheria hiyo inafanya kazi hata kwa watu wenye uraia wa nchi mbili ambao uraia mmojawapo ukiwa unatokana na nchi ambayo raia wake wamezuiwa kuingia Marekani basi mtu huyo ataathirika.
Mfano, raia wa Uingereza mbaye pia ni raia wa Somalia, hatoruhusiwa kuingia Marekani.