Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Uganda, Milutin ‘Micho’ Sredojevic ametishia kujiondoa kwenye timu endapo hatolipwa stahiki zake za malimbikizo ya mishahara.

Micho aliyeweka rekodi ya kufanikiwa kufuzu na timu hiyo kwa michuano ya AFCON baada ya miaka 39 ambayo hata hivyo wametolewa kwenye hatua ya makundi amekilaumu chama cha soka cha Uganda FUFA kwa kushindwa kutekeleza wajibu wake wa mkataba.

Kocha huyo raia wa Serbia ambaye alishawahi kuifundisha miamba ya soka Tanzania, timu ya Yanga ya Dar es Salaam amelalamika kuwa anakidai chama cha soka cha Uganda mishahara yake ya miezi kadhaa.

‘Bila kuungwa mkono na serikali, kama tukiweza kutatua tatizo lililopo kwa uungwana ni vyema na bora. Lakini tukishindwa kufanya hivyo, nasikitika, itanipasa kuchukua hatua za kisheria’.

Uganda imetolewa kwenye michezo ya AFCON kwa kupoteza mechi zake dhidi ya Ghana na Misri huku ikifanikiwa kupata suluhu dhidi ya Mali.

Mkataba wa Micho na timu ya taifa ya Uganda unamalizika mwaka 2019.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *