Mwanaume mmoja mkazi wa Pugu Kinyamwezi, Mohamed Maulid na mtoto wake Sumaiya Mohamed mwenye umri wa miaka mitatu wamemwagiwa mafuta ya moto na mke wake baada ya mke huyo kupewa talaka.
Maulid alisema baada ya kumpa mwanamke huyo talaka alikuwa anampiga tu tarehe kuwa ‘ntaondoka kesho, ntaondoka kesho.’ “Na nilivyokuwa naenda kazini nilimuuliza utaondoka saa ngapi akasema ataondoka jioni, nikahisi kwamba anaona aibu kuondoka mchana ataondoka jioni,”.
Amendelea kusema kuwa “Nilikuwa nimelala nikasikia kama moto umelipuka, nilikuwa nimelala fofoFo, nikashtuka nikaanza kupiga kelele nimemwagiwa maji ya moto nikapiga kelele majirani wengine wakanisikia wakatoka nje, wakaenda kumuangalia na mtoto wakakuta na mtoto naye kaungua sana na yupo kule wodi ya watoto.”