Kundi la al-Shabab wameshambulia kambi ya wanajeshi wa Kenya wanaohudumu chini ya kikosi cha Umoja wa Afrika nchini Somalia.

Wapiganaji hao wanadai kuwaua wanajeshi wengi kwenye shambulio hilo katika kambi ya Kulbiyow kusini mwa Somalia karibu na mpaka wa nchi hiyo na Kenya.

Msemaji huyo amedai kundi hilo limewaua wanajeshi zaidi ya 50 na kutwaa magari na silaha za wanajeshi hao, taarifa ambazo msemaji wa majeshi ya Kenya amekanusha.

Al-Shabab wamekuwa wakipigana dhidi ya serikali ya inayoungwa mkono na mataifa ya magharibi na jamii ya kimataifa.

Wanajeshi wa Kenya pamoja na wanajeshi kutoka Djibouti, Uganda na Ethiopia, chini ya Amisom, wamekuwa wakisaidia serikali hiyo yenye makao yake Mogadishu.

Januari mwaka uliopita, wapiganaji wa al-Shabab walishambulia kambi ya majeshi ya Kenya el-Adde na kuua wanajeshi wengi.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *