Waziri wa Nchi ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), George Simbachawene amesema kuwa mradi wa Mabasi ya Mwendokasi (UDART) umekusanya Sh bilioni 19 toka uanze mwezi Mei mwaka jana.

Simbachawene amesema mradi huo kwa sasa unahudumia abiria wapatao 200,000  na mapato yake yamekuwa yakiongezeka  kila mwezi.

Amesema katika miezi miwili ya mwisho Novemba na Desemba makusanyo yalizidi kuongezeka na kufikia Sh bilioni 3 kwa mwezi.

Amesema katika mchanganuo wa fedha hizo  mpaka sasa msimamizi wa miundombinu hiyo ambao ni UDART wanalipwa Sh milioni 8.1 kwa siku.

Amesema awali UDART ilikuwa ikilipwa Sh milioni 4.4  kabla ya bodi ya usimamizi ya mradi huo kufanya marekebisho baada ya uchunguzi .

Waziri Simbachawane amesema mradi huo una wabia wengine ambao wapo kwenye uendeshaji wa mabasi yake ambao ni UDART, mkusanyaji wa mapato Max Malipo, Benki ya NMB ambao ni wawezeshaji.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *