Mahakama kuu ya Ugirki imetoa uamuzi wa kukataa kuwarudisha nchini Uturuki wanajeshi nane wa nchi hiyo wanaotuhumiwa kuhusika na jaribio la mapinduzi lilishindwa.

Wanajeshi hao wanadaiwa kutoroka kwa helikopta hadi Ugiriki baada ya jaribio la mapinduzi lakini wakadai kuwa hawahusiki na jaribio hilo.

Jaji mkuu wa mahakama hiyo, Giorgos Sakkas alisema kuwa wanajeshi wasingepata hukumu ya haki nchini Uturuki.

Hata hivyo Uturuki imetoa tamko lake na kudai kuwa uamuzi huo wa mahakama kuu una viashiria vya utashi wa kisiasa.

‘Tunapinga uamuzi huu ambao unazuia watu hawa waliotishia maisha ya rais wetu na kusababisha vifo vya watu 248 kuweza kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria vya Uturuki’. Imesema taarifa ya waziri wa mambo ya nje wa uturuki.

Hata hivyo waziri wa sheria wa Uturuki, Stavros Kontonis alisema kabla ya hukumu hiyo kuwa hatoaingilia maamuzi ya mahakama na badala yake atayaheshimu.

Uturuki imewata wanajeshi hao wenye vyeo vya meja, kapteni na sajenti meja iliyowwaita wasaliti warudishwe Uturuki ili wakasikilize kesi yao nchini kwao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *