Wapiganaji wa kundi la Al-Shabab wamewaua wanajeshi wake watatu kwa tuhuma za kufanya upelelezi kwa niaba ya shirika la kijasusi la Marekani (CIA) pamoja na nchi ya Kenya.

Waliouawa Abdullahi Damey Mohamed Nur, 36, Mohamed Iman Hassan, 42, na Mohamed Sharif Ali, 21 wanadaiwa kupokea kati ya $100 hadi $200 kwa mwezi kwa kazi hiyo.

Jaji wa mahakama ya kiislamu ya Al-Shabab amesema kuwa Abdullahi Damey Mohamed Nur alikiri kufanya kazi hiyo kwa niaba ya CIA na alikuwa akilipwa $200.

Taarifa hizo zilizotolewa na mtandao wa Somali Memo ambao unadaiwa kuunga mkono harakati za al-Shabab umeeleza kuwa watu hao waliuawa mbele ya umati mkubwa wa watazamaji kwenye mji wa Yaq-Barawe.

Mohamed Iman Hassan, amenyongwa kwa kudaiwa kufanya upelelezi kwa niaba ya serikali ya Kenya na alikuwa akilipwa $150.

Wakati hao wakidaiwa kuwasaidia CIA na Kenya, Mohamed Sharif Ali, anadaiwa alikuw aakikusanya taarifa kwa niaba ya uongozi wa, Jubbaland.

Mwaka 2011 mhubiri wa kiislam Ahmed Ali Hussein aliuawa na kundi hilo kwa kufungwa minyororo na kupigwa risasi kwa kutuhumiwa kuwa mpelelezi wa CIA.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *