Mwanamume mmoja nchini China alikuwa akiendesha baiskeli hadi nyumbani kwao kusherehekea mwaka mpya, aligundua baada ya siku 30 kuwa alikuwa amepotea njia.

Mwanamume huyo alikuwa na matumaini ya kuwasil nyumbani kwao huko Qiqihar mkoa wa Heilongjian baada ya kuanzia safari yake Rizhao umbali wa kilomita 1,700.

Lakini alisimamishwa na trafiki akiwa amepotea umbali wa kilomita 500 katika mkoa wa Anhui.

Ripoti zinasema kwa mwanamume huyo alikuwa akilala maduka ya intaneti kwa sababu hakuwa na pesa.

Mwanamume huyo hakuwa na uwezo wa kusoma ramani na hivyo alikuwa akitegemea watu kumuelekeza.

Polisi walimsimamisha kwa sababu alikuwa akitumia barabara ambayo baiskeli haziruhisiwi kuitumia.

Baada ya kugundua makosa yake, polisi na watu wote waliokuwa kituoni ambapo alisimama walichanga pesa na kumnunulia tikiti ili asafiri nyumbani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *