Rambirambi za msiba wa mwandishi mkongwe wa vitabu vya fasihi raia wa Nigeria, Buchi Emecheta, zimeendelea kumiminika kufuatia kifo chake nchini Uingereza.
Emecheta alikutwa na umauti akiwa na miaka 72.
Emecheta ambaye ni mmoja wa waandishi wakongwe wa fasihi kutoka Nigeria, ameacha hazina ya vitabu zaidi ya 20 vikiwemo The Joys of Motherhood, Second-Class Citizen, The Bride Price na The Slave Girl.
Pia Emecheta amewahi kushinda tuzo nyingi za uandishi.
Kwa mujibu wa kitengo cha uhusiano na uendelezaji utamaduni wa mwingereza cha British Council, vitabu vingi vya Emecheta vilikuwa vinalenga zaidi siasa na mapenzi na ubaguzi wa rangi huku vingi vikiangazia zaidi maisha yake binafsi.
Moja kati ya matukio makubwa ya kukumbukwa ya Emecheta ni kitendo cha kuachana na mumewe kwasababu alikataa kusoma kitabu chake cha kwanza na kuuchoma moto muongozo wa kitabu hicho.