Southampton wamefanikiwa kuingia fainali ya michuano ya kombe la ligi nchini England (EFL) baada ya kuifunga Liverpool 1-0 kwenye mechi ya mzunguko wa pili iliyofanyika jana usiku katika uwanja wa Anfield.

Goli pekee kwenye mechi hiyo limefungwa na mshambuliaji Shane Long katika dakika ya 90 ya mchezo huo.

Katika mchezo wa nusu fainali ya kwanza Liverpool walifungwa kwa bao moja kwa bila hivyo Southampton wanawatoa kwa jumla ya mabao 2-0.

Nusu fainali nyingine ya pili inachezwa leo hii ambapo Hull City watacheza dhidi ya Manchester United, katika mchezo wa kwanza United walishinda kwa mabao 2-0 .

Mechi wa fainali inatarajiwa kufanyika Februari 26 mwaka huu katika uwanja wa Wembley nchini Uingereza.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *