Rais wa Marekani, Donald Trump amesema serikali yake itaanza mara moja kushughulikia ujenzi wa ukuta kati ya Marekani na Mexico.

Hatua hiyo ni utekelezaji wa ahadi yake kubwa aliyoiweka wakati wa kampeni za uchaguzi nchini Marekani.

Donald Trump amesema ukuta huo utazuia wahamiaji haramu na wafanyabiashara wa dawa za kulevya, kwa kuongeza kuwa siku zao zimekwisha wao kuishi na kufanya uharibifu.

Amesisitiza kauli yake ya kutaka Mexico kulipia ukuta huo, licha ya Mexico kukataa kufanya hivyo.

Kwa upande wake Rais wa Mexico, Enrique Pena Nieto naye anashinikizwa kufuta mkutano wake na Rais Trump unaotarajiwa kufanyika wiki ijayo mjini Washngton, ikiwa kama ni kujibu uamuzi huo wa Marekani kujenga ukuta.

Meya wa mji wa Mexico City Miguel Espinosa amesema kujengwa kwa ukuta huo, Marekani itajitenga yenyewe sio tu na Mexico bali na Amerika ya kusini yote.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *