Mbunge wa Morogoro Mjini, Abdulaziz Abood amekabidhi Sh milioni 48  kwa ajili ya kulipia ada wanafunzi wa elimu ya juu, shule za sekondari na shule za msingi waliopo ndani ya Manispaa ya Morogoro.

Makabidhiano hayo yamefanyika mkoani Morogoro mbele ya wazazi, ambapo Abood amesema suala la elimu linapaswa kupewa kipaumbele kwa kuunga mkono jitihada zinazofanywa na wadau kwa kushirikiana na Serikali.

Pia amesema kuwa hakuna haja ya mzazi na mlezi kuacha ama kushindwa kumpeleka mwanae shule wakati Serikali iliondoa mfumo wa malipo kwa wanafunzi wa shule za msingi  na kuacha majukumu ya kununua sare, mahitaji mengine kwa wazazi na walezi.

Alisema fedha alizotoa  ni kutokana na vyanzo vyake vya mapato huku akiwa amedhamiria kuimarisha elimu hasa kwa watoto, vijana wa jimbo lake kwa kuwasaidia wazazi sehemu ya majukumu yao.

Mbali na hilo mbunge huyo amekabidhi mbao zenye thamani ya Sh milioni 9.8 kwa ajili ya ukarabati wa Shule ya Msingi Kauzeni iliyoezuliwa na mvua kubwa iliyoambatana na upepo mwishoni mwa  mwaka jana.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *