Chombo kinachosimamia usalama nchini Sudani Kusini kimeliomba Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuharakisha kutuma wanajeshi wake wa kulinda amani ili kukabiliana na matukio ya mauaji na uvunjifu wa haki za binadamu.

Vikosi hivyo vinatarajiwa kutumwa kwenye mji mkuu wa Sudani Kusini wa Juba.

Chombo hicho kinasimamia makubaliano ya amani nchini humo pia kimedai kuwa jitihada za kufanyika kwa mdahalo wa pamoja ulioitishwa na rais Salva Kiir utaweza kufanikiwa endapo tu kutakuwa na dhamira ya dhati ya kuwashirikisha wote wanaohusika na mgogoro huo.

Aliyekuwa makamu wa rais na kiongozi wa waasi, Riek Machar ambaye alisaini mkataba huo alilazimika kukimbia nchi hiyo wakati wa mapigano mwezi Julai mwaka jana ambapo mamia ya watu walifariki dunia.

Mapigano ya wenyewe kwa wenyewe nchini humo yamesababisha vifo vya mamia ya maelfu ya watu huku wengine zaidi ya milioni tatu wakikosa mahali pa kuishi na kuwa wakimbizi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *