Shirika la Umeme nchini Tanesco limesema tatizo hilo limesababishwa na hitilafu katika mtambo wa kupooza na kusambaza umeme eneo la Ubungo, Dar es Salaam.
Umeme umekatika muda wa saa kumi na mbili na nusu asubuhi katika maeneo yote yaliyounganishwa na Grid ya taifa isipokuwa baadhi ya maeneo ambayo ayapo kwenye mfumo wa Grid ya taifa.
Kaimu meneja uhusiano wa Tanesco, Leila Muhaji amenukuliwa amesema wataalam wanaendelea kushughulikia tatizo hilo ili umeme urudi katika hali yake ya kawaida na wananchi kupata umeme kama kawaida.
Tatizo hilo la umeme limeathiri baadhi ya taasisi kama vile Dawasco kutokana na kushindwa kusambaza maji kutokana na mitambo yao ya Ruvu Juu na Ruvu Chini kuzima kwa kukosa umeme kabisa.