Mtu mmoja amefariki dunia na wengine 32 kujeruhiwa vibaya baada ya basi la Vitu Laini linalofanya safari zake kutoka vijiji vya Kilolo kwenda Iringa Mjini kugongana na lori la mbao karibu likiwa limekaribia kufika Iringa Mjini.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, ACP Peter Kakamba amethibitisha kutokea kwa ajli hiyo na kueleza kuwa majeruhi wote wa ajali hiyo wamelazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Iringa.

Kuhusu chanzo cha ajali hiyo haijafahamika kama ni matatizo ya gari au mwendoksasi wa dereva hivyo Kamanda Kakamba amesema watatoa taarifa rasmi baabdaye kuhusu tukio hilo.

Ajali za barabarani ni janga la taifa kwa sasa kutokana na kupoteza uhai wa raia au kupata ulemavu wa maisha kutokana na ajali hizo ambapo muda mwingine ajali hizo zinasababishwa na uzembe wa madereva.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *