Mtandao wa Shirikisho la soka barani Afrika (CAF) umedukuliwa na kundi la Urusi New World Hackers wakidai kupinga Gabon kuandaa michuano ya Mataifa ya Afrika (Afcon) mwaka huu.

Wanachama wa kundi hilo waliiambia wamesema kuwa walifanya hivyo kupinga Gabon, kuwa mwenyeji wa michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika huku wakisema Gabon ni nchi ya udikteta.

Shirikisho la soka barani Afrika (CAF) limeongeza shughuli ya sekunde tano ya kuwachunguza wageni wote kwenye mtandao wake, ifahamikayo kama Cloudflare, kama njia ya kukabiliana na tatizo hilo.

Mtandao wa CAF ulifungwa kwa saa tano siku ya Jumamosi, na kusababisha viongozi wa bodi hiyo kuchunguza hitalafu ya kimtandao wakidhani ilikuwa chanzo, kabla ya kubaini tatizo lilitokana na udukuzi

Mwaka huu michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika imepingwa na raia kadhaa wa Gabon ambao wametumia nafasi hiyo kuelezea malalamiko yao ya kisiasa.

Siku ya Jumapili New World Hackers, pia walidai kudukua mtandao wa kampuni ya mafuta ya Total, ambayo ilitangaza udhamini mkubwa wa mamilioni ya dola kwa CAF mwaka jana.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *